JavaScriptSDK

Monday, March 20, 2017

KHUDDAMUL AHMADIYYA WAENDESHA BAISKELI NA KUGAWA VIPEPERUSHI KUAZIMISHA SIKU YA MASIHI ALIYEAHIWA a.s.


Majlis Khuddamul Ahmadiyya mkoa wa Dar Es Salaam wameshiriki katika zoezi maalumu la matembezi ya baiskeli na kugawa vipeperushi katika kuadhimisha siku ya Masihi Aliyeahidiwa ambayo hufanyika ifikapo Machi 23 ya kila mwaka.

Matembezi hayo yaliwashirikisha pia viongozi wa Majlis Mulk ya Khuddamul Ahmadiyya akiwemo Sadr sahib.

Wakiwa wamevalia vizibao maalumu (reflectors) zenye ujumbe wa ISLAM FOR PEACE yaani ISLAMU KWA AMANI, msafara ulianzia Masjid Salaam mnamo saa 3:00 asubuhi baada ya maombi yaliyoongozwa na Amir na Mbashiri wa Jamaat Ahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, ukiingilia barabara ya Bibi Titi Mohammed kuelekea barabara ya Lumumba pamoja na gari mbili, moja iliyotangulia mbele kuongoza na nyingine ilibaki nyuma kuhakikisha hali usalama kwa waendesha baiskeli wetu.




Kutoka Mtaa wa Lumumba, msafara ulipitia barabara ya Uhuru ambapo zoezi la ugawaji vipeperushi lilifanyika kwa takribani dakika 10 likiongozwa na Sadr Sahib.
Baadae msafara ulisimama katika soko la Karume kisha Keko ambapo watu kadhaa walijitokeza kutaka kujua lengo la msafara wetu ambao kwa muda wote wa safari zilisikia sauti za Takbira na Tashahhud kutoka kwa vijana waliokuwa na hamasa ya aina yake.


Baadae msafara uliendelea ukipita katika barabara ya Changombe, Kilwa Road, Gerezani, Stesheni na baadae kurejea katika barabara ya Bibi Titi Mohammed yalipo Makao makuu ya Jamaat.



 Kila jambo jema halikosi changamoto. Moja ya matukio ya kukumbukwa ni kitendo cha askari wa Barabarani wakishirikiana na Polisi wa Usalama kuusimamisha msafara wa waendesha baiskeli wetu katika eneo la bandari wakidhani kuwa tulikuwa katika mgomo fulani. Baada ya mazungumzo ya muda mfupi na viongozi wa Khuddam msafara uliruhusiwa huku Polisi wakifuatilia nyuma hadi Masjid Salaam kuhakikisha kuwa hapakuwa na ajenda nyingine yeyote zaidi ya matembezi ya Amani.

Tukio hilo la uendeshaji baiskeli liliwachukua Khuddam kiasi cha saa moja na dakika 10 ambapo walikamilisha umbali wa Kilomita 10.73 za kuzunguka katika barabara za manispaa ya Temeke na Ilala.


Kitaifa na kimkoa, maadhimisho ya Siku Masihi Aliyeahidiwa na Mwanzilishi wa Jumuiya ya Waisalamu Waahmadiyya Ulimwenguni Hadrat Mirza Ghulam Ahmad a.s yatafanyika katika viwanja vya Jamaat katika eneo la Kitonga siku ya Jumapili.

Saturday, February 11, 2017

MPANGO WA KUJITOLEA DAMU WAFANA, ALHAMDULILLAH

Kulia: Qaid Ilaqa ya Dar es salaam
Kushoto: Sadr Majlis Khuddamul Ahmadiyya Tanzania
Kwa fadhila za Allah, Majlis Khuddamul Ahmadiyya Ilaqa ya Dar es salaam wamefanikisha tukio la uchangiaji damu lililofanyika katika Ofisi za Damu Salama kanda ya Mashariki kama lilivyotangazwa hapo kabla.

Muhtamim Tarbiyyat katika mchakato wa kutoa damu
Toka Kulia: Qaid Ilaqa, Muhtamim Maal na
Muhtamim Khidmat Khalq katika mchakato wa kutoa damu
Tukio hilo lilihudhuriwa na Khuddam wapatao ishirini na nne (24), akiwemo na Sadr Majlis pamoja na baadhi ya wana Majlis Mulk pia.

Tukio hilo liliambatana na kikao pamoja na uongozi wa Damu Salama kanda ya Mashariki kilichokuwa na madhumuni ya Kufahamiana zaidi na kuzijadili changamoto za pande zote katika Masuala yote yahusuyo damu.









Kabla ya zoezi la utoaji damu kuanzishwa rasmi, washiriki waote walipata maelekezo ya mazingira na Kufahamishwa shughuli za idara kadhaa zilizopo hapo.

 







#KhidmatKhalq        @ChangiaDamuTZ    #GiveBlood     #BelieveInGiving   #OkoaMaisha

Monday, February 6, 2017

MPANGO WA KUJITOLEA DAMU

Mnamo tarehe 11 Februari 2017 kutakuwa na tukio la kujitolea damu  Makao makuu ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS). Tukio hilo lililoandaliwa na Majlis Khuddamul Ahmadiyya, Ilaqa ya Dar es salaaam litafanyika kuanzia majira ya saa 1 na dakika 30 asubuhi.


Wanajumuiya wote watakaokuwa na wasaa wanaombwa washiriki kwa pamoja katika zoezi hili adhimu.

Eneo husika la tukio linavuma kwa jina la kituo cha mabasi "MSIMBAZI CENTRE". Mwisho wa makala hii kuna ramani ya Google inayoonyesha kwa uchache mahali husika.

Hakika kuna faida za Kitabibu za Utoaji damu. Takwimu zinaonyesha 25% yetu tutahitaji kuwekewa damu nyakati fulani katika maisha yetu. Baadhi ya faida hizo ni:

  • Husababisha mwili kuzalisha seli mpya zenye afya za damu.
  • Hupunguza mzigo wa madini ya chuma mwilini hivyo huchukua nafasi katika kuzuia ugonjwa wa moyo.
  • Kuna uwezekano kidogo wa kupata magonjwa ya moyo na unene wa kupitiliza. Wanaume wanaoshiriki uchangiaji damu wana hatari chini ya 30% ya kupata magonjwa ya moyo na kupooza.
  • Tunapochangia damu chupa moja, miili yetu hupunguza Kalori 650.

Allah Atujaalie tupate fadhila Zake na kujichumia faida za kiafya za zoezi hili. Aamiin!