Mnamo tarehe 11 Februari 2017 kutakuwa na tukio la kujitolea damu Makao makuu ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS). Tukio hilo lililoandaliwa na Majlis Khuddamul Ahmadiyya, Ilaqa ya Dar es salaaam litafanyika kuanzia majira ya saa 1 na dakika 30 asubuhi.
Wanajumuiya wote watakaokuwa na wasaa wanaombwa washiriki kwa pamoja katika zoezi hili adhimu.
Eneo husika la tukio linavuma kwa jina la kituo cha mabasi "MSIMBAZI CENTRE". Mwisho wa makala hii kuna ramani ya Google inayoonyesha kwa uchache mahali husika.
Hakika kuna faida za Kitabibu za Utoaji damu. Takwimu zinaonyesha 25% yetu tutahitaji kuwekewa damu nyakati fulani katika maisha yetu. Baadhi ya faida hizo ni:
- Husababisha mwili kuzalisha seli mpya zenye afya za damu.
- Hupunguza mzigo wa madini ya chuma mwilini hivyo huchukua nafasi katika kuzuia ugonjwa wa moyo.
- Kuna uwezekano kidogo wa kupata magonjwa ya moyo na unene wa kupitiliza. Wanaume wanaoshiriki uchangiaji damu wana hatari chini ya 30% ya kupata magonjwa ya moyo na kupooza.
- Tunapochangia damu chupa moja, miili yetu hupunguza Kalori 650.
Allah Atujaalie tupate fadhila Zake na kujichumia faida za kiafya za zoezi hili. Aamiin!
No comments:
Post a Comment