Khuddam-ul
Ahmadiyya ni Tanzimu au Tawi la Vijana wa Kiislamu wa Jumuiya ya Waislamu Wa-Ahmadiyya
Duniani. Tanzimu au Tawi hili ni la vijana wa Kiahmadiyya kuanzia miaka 15 mpaka
40. Khuddam-ul Ahmadiyya ilianzishwa rasmi na Khalifatul Masih II, Hadhrat
Mirza Bashiruddin Mahmood Ahmad (ra) mwaka 1938. Kulingana na Khalifatul Masih
II, maneno Khuddamul Ahmadiyya
maana yake vijana waliopo katika kundi hili ni Watumishi wa Ahmadiyya. Katika hotuba yake yenye kukumbukwa
sana aliyoitoa Aprili 1, 1938, katika
msikiti wa Al Aqsa uliopo Qadian, India, Khalifatul Masih II (ra):
Khalifatul Masih II(ra), Mwanzilishi wa Majlis Khuddamul Ahmadiyya |
“Nimekuwa nikisisitiza jumuiya kuhusiana na
ukweli kwamba, Kuimarika kwa Taifa Lolote Hakuwezi Kutimia Pasipo Vijana Wake
Kuwa Imara.Jumuiya yetu haiwezi kupata maenedeleo ya kweli mpaka pale vizazi
vipya havijatekeleza Ujumbe na Mafundisho sahihi Kiislamu ambayo Mtume S.A.W
aliyaleta Duniani. Khuddamul Ahmadiyya maana yake ni Watumishi wa Ahmadiyya. Jina
hili daima litaendelea kuwakumbusha kwamba wao ni watumishi, na si kutumikiwa.
Mnatakiwa mdhihirishe na muimarishe vipawa
vyenu kwamna iliyo bora. Ikiwa mtaonesha mfano mwema kwa wengine, itakuwa
rahisi kuwavutia kujiunga na jumuiya yenu.”
Bendera rasmi ya Majlis Khuddamul Ahmadiyya ambayo inatumiwa na vijana wa Ki-Ahmadiyya kuanzia miaka 15 hadi 40 |
Majlis Khuddamul Ahmadiyya Tanzania ni sehemu ya kauli hiyo ya
Khalifatul Masih II (ra) kwani madhumuni ya kuanzishwa kwake yanabeba maana
nzima ya Utumishi si kwa Jumuiya pekee bali utumishi kwa viumbe vyote vya Allah
kwa lengo la kupata radhi yake.
ITAENDELEA…
No comments:
Post a Comment