JavaScriptSDK

Saturday, May 21, 2016

IJITIMAA YA KHUDDAM TAIFA 2016 INAENDELEA KITONGA...

Leo tar 21 Mei 2016 Ijitimaa ya Taifa ya Khuddamul Ahmadiyya Tanzania inendelea katika katika viwanja vya Ahmadiyya Kitonga nje kidogo ya jiji la Dar. Kauli mbiu ya Ijtimaa ya mwaka huu kama ilivyo miaka yote ni; 'TAIFA HALIWEZI KUWA IMARA BILA KWANZA KUWAIMARISHA VIJANA WAKE'. Vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na nchi majirani zikiwemo Kenya na Uganda wanajumuika kwa muda wa siku tatu za Sala, Maombi na Mashindano mbalimbali ya michezo na kielimu ambapo vijana hao wanapata fursa ya kujuana, kujadiliana na kujifunza mambo yahusuyo dini ya Islam na maisha kwa ujumla.
Kwa kawaida siku hizi tatu za Ijitimaa huwa na faida kubwa kiroho kwa washiriki kwani pia hupata fursa ya kuswali sala ya kisimamo cha usiku (TAHAJJUD) kwa pamoja kwa muda wote watakaokuwa mahali hapo.
Watu kutoka dini zote wanakaribishwa katika Ijitimaa ya Khuddamul Ahmadiyya Tanzania 2016.
Wageni waalikwa kutoka madhehebu ya dini zote, viongozi wa serikali na watu binafsi ni moja ya waalikwa na watoa mada katika Ijitimaa hii. Hivyo, ni vyema ukahudhuria na kujumuika pamoja vijana wa Kiahmadiyya na ujufunze mengi.

No comments: