HADRAT MIRZA GHULAM AHMAD (A.S) Mwanzilishi Mtukufu Wa Jumuiya Ya Waislamu Waahmadiyya Duniani |
BISHARA kuhusu ujaji wa Kiongozi mkubwa kiroho hupatikana katika dini zote takriban. Na huu ndio wakati ambapo wafuasi wa dini zote wanamngoja huyo Kiongozi kwa hamu na kiherehere.
Kwa kuwa bishara hizo zimeiajwa kwa uwazi
zaidi katika vitabu vya Kiislamu na vya Kikristo, hivyo twapenda kueleza
habari hii kulingana na dini hizo mbili.
Waislamu kwa Wakristo wanaamini kwamba Nabii
Isa (a.s.) au Yesu Kristo atashuka kutoka mbinguni. Jambo la muhimu kuhusu
habari hii ni kwamba Nabii Isa (a.s.) hakufa msalabani wala hakupaa mbinguni,
bali alikufa kifo cha kawaida. Na anayekufa harudi duniani tena. Hivyo,
swali la kurudi Nabii Isa (a.s.) wa zamani haliwezi kuzuka.
Muradi wa bishara kuhusu kuja kwa Nabii
Isa (a.s.) mara ya tena, ni kwamba mwingine aiakayefanana naye atakuja
na kwa njia hii bishara itaiimia.
Hakika yenyewe ni kwamba kufika mara ya
pili kwa Mtume wa zamani katika lugha ya kidini kunamaanisha kwamba mtu
mwingine atakayefanana naye kiroho atafika. Nabii Isa (a.s.) ambaye bishara
ya kuja kwa Masihi aliyeahidiwa inamhusu yeye moja kwa moja, mwenyewe
atifafanua jambo hili kwa uwazi sana.
Nabbii Isa (a.s.) alipodai kuwa yu Masihi,
Mayahudi walipinga wakisema, Eliya aliyepanda mbinguni (2-Wafalme 2:11)
ateremke kwanza kutoka mbinguni. Lakini Nabii Isa (a.s.) aliwafahimisha
kwamba habari ile ilikuwa ni mithali tu na hakika yake ni kwamba angefika
mtu mwingine akifanana na Eliya.
Kasema Nabii Isa (a.s.): "Kweli Eliya
atakuja ayaweke mambo yote katika mpango, lakini nawaambieni, Eliya amekwisha
kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Adamu
atateswa vivyo hivyo mikononi mwao. Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba
alikuwa akiwaambia juu ya Yohana Mbatizaji (Mathayo 17:11-13).
Nabii Isa (a.s.) kwa kuwatolea wafuasi wake
mfano huu, aliwafahamisha kwamba kama vile bishara ya kufika Eliya ilivyotimia
katika dhati ya Yohana Mbatizaji, hivyo ndivyo itakavyokuwa kujt) kwake
mara ya pili. Yaani si yeye mwenyewe atakayekuja. bali mfano wake yeye
atafika,
Si hayo tu, bali Mtume Mtukufu Muhammad
S.A.W, aliyetabiri ufikaji wa Masihi, alisema kwa uwazi sana kwamba Masihi
atatokea katika Waisiamu. Alivyosema Mtume S.A.W, ni kwamba, "Mtakuwaje
aiakapofika Mwana wa Mariamu kati yenu, naye atakuwa Imam wenu kutoka
miongoni mwenu..." (Bukhari). Maneno "KUTOKA MIONGONI MWENU"
yanahakikisha wazi kabisa kwamba Masihi aliyeahidiwa, atatokana na Waislamu
ambaye; atazaliwa katika Waislamu.
Tungependa kuwapasha wanadamu wote habari
njema kwamba yule Kiongozi aliyetazamiwa kufika, aliyekuwa akingojewa
kwa hamu na kiherehere na mataifa yote, amekwisha fika tayari, naye ndiye
Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad wa Qadian, India (1835-1908),
Waahamadiyya, Ametumwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu wote kwenye
dini ya kweli nayo ndiyo ISLAM. Ni mwana wa kiroho wa Mtume Mtukufu Muhammad
S.A.W. aliyepata cheo cha Unabii katika utii na ufuasi kamili wa Bwana
wake Muhammad S.A.W.
Twataka kusema maehache juu ya ukweli wa
Mwanzllishi Mtakatifu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya. Kurani Tukufu
yatuambia kwamba Mitume wa Mungu daima hushinda (58:22), Na vile vile,
Intuhakikishia kwamba mwenye kumzuilia Mungu uwongo sio tu kwamba ananyimwya
msaada wa Mungu, bali hupata adhabu kutoka kwa Mungu (69:45-48). Kununi
hii ya mwongo kuadhiniwa imetajwa katika Biblia pia (Kumbukumbu 18:20;
13:5).
Ijapokuwa Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (a.s.)
alikabili upinzani mkali kutoka kwa Waislamu, Wakristo na wafuasi wa dini
nyingine, lakini ni yeye aliyepata ushindi na kufaulu kwa msaada wa Mwenyezi
Mungu na leo hii sauti yake inasikika katika dunia nzima na Jumuiya Ahmadiyya
kwa fadhili za Mwenyezi Mungu imesitawi katika nchi zaidi ya 130. Kinyume
chake,wapinzani wake walishindwa na kufedheheka nao wanaendelea kufedheheka
hadi leo. Wako wapi akina Bhutto na Zaia-ul-Haq wa Pakistan na Idi Amin
wa Uganda?
Mtukufu Mtume Muhammad S.A.W. vile vile
alitabiri kutokea ishara mbili za maana sana wakati atakapokuja Masihi
na Imam Mahdi. Mtume S.A.W. alisema: "Hakika kwa ajili ya Mahdi wetu
kuna ishara mbili ambazo hazijapata kutokea tangu kuumbwa mbingu na ardhi,
nazo ni: "Mwezi utapatwa usiku wa kwanza katika Ramadhani, na Jua
litapatwa katikati katika mwezi huo" (Dar Qutni, J.I. Uk.188). Tena,
ishara hizi zimetajwa hata katika vitabu vya zamani zikiwa ishara za kufika
Yesu mara ya pili, kama yeye Yesu mwenyewe alivyosema: "Lakini mara,
baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga
wake" (Mathayo 24:29).
Ishara hizo za kimbinguni zilitimia mnamo
mwaka 1894(1311 A.H.) ambapo katika Ramadhani mwezi ulipatwa ya kwanza
katika tarehe za kupatwa kwake yaani 13 na Jua likapatwa terehe ya katikati
yaani tarehe 28.
Mwanzilishi Mtakatifu wa Jumuiya Ahamadiyya
alopodai kuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu na kwamba yu Imam Mahdi, Masheik
wa India walimpinga vikali wakisema, "Mbona zile alama za kupatwa
Jua na Mwezi katika Ramadham zilizotajwa kaiika Hadithi ya Mtume S.A.W.
hazikutimia?" Lakini ajabu ni kwamba atama hizo zilipotimia, Masheikh
wale wale walianza kupiga kelele wakisema, "sasa watu watapotea".
Walikuwa na maana kwamba ishara za ukweli wa Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad
(a.s.) zimetimia tayari, hivyo watu watamwamini na kujiunga na Jumuiya
yake.
Kwa neno zima, bishara ya kuhusu ujaji wa
Masihi na Imam Mahdi imekwisha timia tayari katika dhati tukufu ya Hadhrat
Mirza Ghulam Ahmad (a.s.). Mwenye masikio na asikie. Kama si yeye, ni
nani aliyetokea badala yake? Au, je, mtaendelea kumngoja yule Masihi Mnazareti
kama vile Mayahudi wanavyoendelea mpaka leo kumngoja Eliya ashuke kutoka
mbinguni, lakini yeye haji wala hatakuja kamwe. Hivyo ndivyo mtakavyoendetea
kumngoja Nabii Isa (a.s.) mwenyewe atokee mpaka mtachoka, lakini yeye
hatakuja katu.
Mwanzilishi Mtakatifu wa Jumuiya ya Waislamu
Waahmadiyya, Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (a.s.) akitabiri, alisema mnamo
mwaka 1903: "Kumbukeni, hakuna atakayeshuka kutoka mbinguni. Wapinzani
wetu wote walio hai wakati huu, watakufa wala hakuna hata mmoja kati yao
atakayeshuhudia Isa bin Mariam kuteremka kutoka mbinguni. Kisha kizazi
chao kitakachobaki nacho kitakufa wala hakuna yeyote atakayeona Isa bin
Mariam kushuka kutoka mbinguni. Bali kizazi cha kizazi hicho nacho kitakufa
bila kushuhudia mwanaye Mariam kushuka kutoka mbinguni. Hapo Mungu Atawatilia
wasiwasi na mahangaiko nyoyoni mwao kwamba zama za ushindi wa msalaba
zimekwisha pita na dunia imeingia katika hali tofauti, lakini mtoto wa
Mariam hajashuka bado kuioka mbinguni. Hapo mara moja wenye busara wataachana
na imani hiyo".
No comments:
Post a Comment