Yesu Kristo anasema; "Msidhani ya kuwa
nilikuja kuitangua Torati au Manabii, la, sikuja kutangua, bali kuitimiliza.
Kwa maana nawaambieni, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja na
nukta moja ya Torati haitaondoka mpaka yote yatimie (Mathayo 5:18-18)"
Ni dhahiri kuwa Nabii Musa na manabii wengine
watiotangulia walkuja kuwafundisha na kuwaongoza Waisraeli tu. Yesu Kristo
amekwisha kubali katika maneno ya juu ya kuwa amekuja kulitimiza kusudi
lile ile ya Musa na Manabii wengine waliotangulia.
Lakini tunaona mapadri wamekwisha fika katika
kila sehemu ya dunia hata Afrika ijapokuwa Yesu Kristo mwenyewe hakuwa
na nia na kusudi ya namna hii kabisa. Sasa swali hasa linalotakiwa kufikiriwa,
si Wakristo wanafanya nini, bali ni, "Je, Yesu Kristo alikuwa na
nia na azimio gani?" Mwenyezi Mungu alikuwa na kusudi gani alipomtuma
Yesu Kristo? Jambo hili haliwezekani kuelezwa kwa njia nzuri na yeyote
isipokuwa lielezwe na Yesu Kristo mwenyewe. Na Yesu amekwisha sema wazi
"Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt.
15:24). Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoka kilichopotea
(Matt. 18:11)."
Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa
ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa. Inasemekana kwanba Yesu
Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa, Inasemekana
kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia.
"Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza
kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"
Lakini kushika dalili katika maneno haya
kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu
wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa. Maana Yesu Kristo amesema wazi
kabisa:
"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi
mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu
katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara.
Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19). ‘Tena, "Sikupelekwa
ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24). "Tena,
Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26) "Sio
haya tu bali pia tunasoma, "Hawa thenashara Yesu aliwatuma akawaagiza,
akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie;
Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt.
105-6)""
Kutoka kwa mafungu ya maneno haya ni kuwa
wafuasi wake wameamrishwa naye kupeleka ujumbe wake kwa mataifa yote ya
Israeli si mataifa yote ya ulimwenguni. Mtu asidhani ya kwamba mawazo
ya maneno yajuuni kuwa waende kwanza miji ya Waisraeli na baadaye kwenye
miji mingine. La, maana kwenda kwa kondoo waliopotea wa Israeli si maana
yake kuvitazama vijiji tu, bali ni kuwaingiza katika dini ya Ukristo.
Basi kwa hakika maana hasa ya maneno haya ni kuwa Waisraeli wote waingie
katika Ukristo, Mkristo na padri ye yote asijielekeze kabisa kwenye mataifa
mengine. Yesu Kristo amehakikisha wazi wazi ya kuwa kazi ya kuwahubiria
dini Waisraeli na kuwaingiza katika njia yake haitamalizika mpaka kufika
kwake mara ya pili, kama ilivyosema:
"Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni
mwingine kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza mji yote ya Israeli
hata ajapo mwana wa Adamu (Matt.10:23). "Katika maneno haya inajulikana
wazi ya kuwa yaliyosemwa katika Mathayo (28:19) makusudio yake ni kwamba
wahubiri Wakristo wasimamishe Ukristo katika miji ya Israeli na waingize
kabila la Israeli katika dini yao si kuvitembelea tu na kuvitazama vijiji
vya Waisraeli. Na pia ni wazi ya kuwa kazi hii ya kuhubiri na kuwaingizia
haitamalizika mpaka Yesu Kristo aje mara ya pili. Kwa hiyo kuwahubiri
watu wengine wasio katika mataifa ya Israeli ni kinyume kabisa na mafundisho
na maagizo ya Yesu Kristo. Hata mitume wa Yesu pia walifahamu kuwa ni
kosa kuwahubiri watu wengine wasio Waisraeli. Tunasoma:
Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika
zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu.
"Basi wale waliotawanyika kwa sababu
ya ile shida iliyotokea kwa habari ya Stefano wakasafiri hata Foiniki
na Kupro na Antiokia. Wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao!!
(matendo11:19)." Hivyo, mitume wa Yesu waliposikia ya kuwa Petro
aliwahubiri watu wasio Israeli pahali fulani, wakakasirikia nawakashindana
naye:
"Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi,
wale walio wa Tohara wakishindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa
ukala nao" (Matendo 11:2-3)",
Kwa neno zima kabla ya Mtume wetu Muhammad (saw) hakuna
nabii au mtume ye yote aliyeamrishwa na Mwenyezi Mungu kuwahubiri watu
wote wa ulimwengu mafundisho yake. Wao walikuwa wanatumwa kwa makabila
maalumu na miji kadha wa kadha. Wala hakuna dalili yoyote ihakikishayo
ya kuwa Yesu Kristo alitumwa kwa makabila yote ya dunia nzima wala hakuna
ishara idhihirishayo ya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wanafunzi wake kuwahubiri
watu wa ulimwengu mzima isipokuwa alisema:
"Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea
wa nyumba ya Israeli (Matt.15:24)," Mapadri wanaofanya kazi ya kuhubiri
dini ya Ukristo katika Waafrika na watu wengine wasio Israeli kwa hakika
wanafanya kinyume cha maagizo ya Yesu Kristo ?
Naam, Mtume Muhammad (saw) kwa amri ya Mwenyezi Mungu alisema:
"Enyi watu wote! Kwa hakika mimi ni Miumbe wa haki niliyetumwa na
Mwenyezi Mungu kwenu nyote" (Kurani 7:159).
TAFSIRI ZA INJILI ZINAPINZANA
Tafsiri ya zamani ya 1 Wakorinto 7:1 ilisema:
"Basi, kwa mambo yale mliyoandika,
ni heri mwanamume asiguse mwanamke."
Na tafsiri mpya ya sehemu hiyo inasomeka hivi:
"Na sasa nataka kuwajibuni juu ya mambo
mliyoandika. Mliniuliza kama ni jambo, nzuri mwanamume asikae na mwanamke."
Tafsiri ya kwanza ina maneno machache. Tafsiri mpya ina
maneno
mengi. Kwa nini?
Na kwa nini.maelezo ya zamani na ya sasa
yamepewa sura ya ulizo? Nenohili: MLINlULlZA limetoka wapi? Wala halimo
katika tafsiri yo yote iliyopata kutangazwa hadi leo?
Hata tafsiri mpya inayoitwa HABARI NJEMA
KWA WATU WOTE haina habari ya MLINIULIZA. Je, mnaharibu maksudi maneno
mnayotuambia ni matakatifu?
Wala hamna faida katika kugeuza tafsiri
ya kifungu cha kwanza. Kwa sababu vifungu vinne vinavyofuata vinasema
nia ile ile ya ubora wa kukaa bila kuoa. Hebu someni chini yake kifungu
cha 7,17, k27, 32, 34, 35, 37 na 40. Mpaka mwisho wa mlango huu wa saba,
Mt. Paul anangang’ania jambo hili hili la kukaa bila kuoa kuwa bora
kuliko kuoa. Sasa mtageuza mlango huu wote ili muwe na mafundisho ya namna
nyingine?
No comments:
Post a Comment